MTU HANA KITU BILA MUNGU ANAPOMFANYA KITU
“Ndipo Daudi, mfalme, akaingia, akaketi mbele za Bwana, akasema, ‘Mimi ni nani, Bwana Mungu, na nyumba yangu ni nini, hata umenileta hata hapa?” (2Samweli 7:18)
“Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.” (Yeremia 1:5)
“Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, ee Yakobo, yeye aliyekuumba, ee Israeli, asema hivi, “Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.” (Isaya 43: 1)
“Je
mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake?
Naama, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau
wewe.Tazama, nimekuchora
katika vitanga vya mikono yangu, kuta zako ziko mbele zangu daima.” (Isaya
49:15-16)
“Wewe uliniona hata kabla sijazaliwa; uliandiika kila kitu kitabuni mwako, siku zangu zote ulizipanga hata kabla ya kuweko ile ya kwanza.” (Zaburi 139:16)
“Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa, ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu, nitakusifu Wewe daima.” (Zaburi 71:6)
“Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha, matendo yako yote ni ya ajabu, na nafsi yangu yajua sana.” (Zaburi. 139: 14)
“Mtu
ni nini ee Mungu hata umfikirie, binadamu ni nani hata humjali, umemfanya mdogo
punde kuliko Mungu, umemvika taji ya utukufu na heshima.” (Zaburi 8:4-5)
“Ee
nafsi yangu, umuhimidi Bwana, naam vyote vilivyomo ndani yangu vilihimidi jina
lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, wala usizisahau fadhili zake zote.”
(Zaburi 103:1-2)
Amina.