Maisha yetu ya leo ndio historia yetu ya kesho, itakayokumbukwa tukiwa hatupo tena hapa duniani.Tulivyo leo sivyo tulivyokuwa jana, tutakavyokuwa kesho ni matokeo ya jinsi tunavyoishi leo.Tuishi vizuri leo tuijenge kesho yetu, ipate kuwa bora zaidi ya leo. Jana itabaki kuwa historia, leo tunaweza kuandika historia ya maisha yetu. Historia nzuri au mbaya ya maisha yetu, ndio itakayotengeneza historia ya maisha yetu ya kesho.Tuishi vizuri leo tuijenge kesho yetu kwa faida ya vizazi vijavyo.Tusisubiri watu waiandike historia ya maisha yetu, tuiandike sasa tukiwa bado hai kwa kuishi vizuri hapa duniani.
"Binadamu hatadumu katika fahari yake, atakufa tu kama mnyama.” (Zaburi 49:12) “Makaburi ni makao yao hata milele, ni makao yao vizazi hata vizazi, ingawa hapo awali walimiliki ardhi.” (Zaburi 49: 11) “Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri, na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.” (Mathayo 7:17-19) Tuishi vizuri leo tuijenge kesho yetu.