Skip to Content

MATANGAZO DOMINIKA YA 23 YA MWAKA A

Jubilei ya Miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam: “Tufanywe Upya kwa Roho Mtakatifu”
5 Septemba 2026 na
MATANGAZO DOMINIKA YA 23 YA MWAKA A
St Peter's Catholic Church, Administrator
| Hakuna maoni bado

1.Tunawashukuru sana Jumuiya ya Mt. Eliya waliosafisha Kanisa jana. Idadi yao ni 7 Wiki ijayo ni zamu ya jumuiya ya Mt. Leo Mkuu watafuatiwa naJumuiya ya Mt. Luka Mwinjili.

2.Jumuiya ambazo hazijawasilisha michango ya 2000/= kwa kila mbatizwa kwa ajili ya Ujenzi wa Kanisa Kuu Mbadala Pugu zinaombwa kukamilisha zoezi hilo. Hali kadhalika wenyeviti wa Jumuiya mnaombwa kuwasilisha orodha ya waamini waliochangia michango hiyo kwa aajili ya kuweka kumbukumbu vizuri.

3.Idara ya Kichungaji ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam inatualika Waamini wote wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam kushiriki Wsrsha maalum itakayofanyika tarehe 26 Septemba, 2026 katika Uwanja wa Uhuru. Lengo la Warsha hizi ni kutuimarisha kiimani na kujenga umoja wa Kisinodi Jimboni kwetu. Aidha, tunaombwa kuchangia ada ya ushiriki ya shilingi 5,000 ambayo itatumika kulipia gharama mbalimbali.Tujiandikishe kupitia Jumuiya zetu

​

4.Kutakuwepo na Semina elekezi kwa wajumbe wa Kamati Tendaji zote za Jumuiya na Kanda Dominika ya tarehe 13/09/2026 mara baada ya Misa ya pili katika Ukumbi wa Kardinali Rugambwa. Tafadhali viongozi tajwa wote mnaombwa kuhudhuria semina hiyo bila kukosa.

5.Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Vincent Lawrence Mpwaji atakuja rasmi kwenye Makazi yake yaliopo katika eneo ka Parokia yetu tarehe 09/09/2026. Atafika saa 10:00 jioni. Ataanzia hapa Kanisani ambapo atasali kwa muda mfupi kabla ya kuelekea kwenye Makazi yake. Masaki. Wanaparokia tunaalikwa kujitokeza kumpokea.

​

6.Leo Watoto wa mafundisho ya Komunio ya Kwanza watapokea Ekaristi Takatifu kwa mara ya kwanza kwenye Misa ya saa 5:15. Hivyo, hakutakuwepo na Misa ya jioni ili kuwawezesha Watoto wengine kuhudhuria Adhimisho hilo la Misa.

7.Tunapenda kuwakumbusha kuendelea kulipa ahadi za Tegemeza Kanisa kwani kilele  cha zoezi hilo kwa mwaka huu kimekaribia sana.

8.Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu sana Jude Thadeus Ruwaichi anatualika kushiriki Adhimisho Takatifu La Hija ya Kijimbo katika kuadhimisha SIKUKUU YA KUTUKUKA KWA MSALABA.

Sherehe itafanyika siku yaJumamosi, 12 Septemba 2026, ikianza naMisa Takatifu saa 3:30 asubuhikatikaKituo cha Hija Pugu.

Kabla ya Misa,Kusikiliza dhambi kutapatikana kuanzia saa 1:30 asubuhi. Baada ya Misa, kutakuwa na maonyesho yanakala halisi ya Mavazi ya Yesu.

9. TANGAZO LA KWANZA LA UPADRE – LA MATESO YA YESU KRISTO

Shemas Richard Seraphine Mlay – Kutoka Parokia ya Chang’ombe.

10.SHIRIKA Mwenye kujua kizuizi awasiliane na Paroko. Zaidi sana tuwaombee

​


TANGAZO LA NDOA

TANGAZO LA KWANZA

  • Anthony Joel Birope na Martha Adam Luhanga
  • Andrew Akilei Macha na Rose Anthony Ndauka
  • Juvenal Ladislaus Kimaro na Neema Paulo Urio
  • James Donald Davisen na Rose Anthony Joachim

TANGAZO LA PILI

  • Oscar Novatus Mbelwa na Rachel Anthony Njawike



ASANTE SANA KWA UKARIMU WENU. MUNGU AWABARIKI NYOTE. 🙏✝️

MATANGAZO DOMINIKA YA 23 YA MWAKA A
St Peter's Catholic Church, Administrator 5 Septemba 2026
Shiriki posti hii
Madaraka
Sign in to leave a comment