Skip to Content

MATANGAZO DOMINIKA YA 28 YA MWAKA A

JUBILEI YA MIAKA 75 YA JIMBO KUU LA DSM; TUFANYWE UPYA NA ROHO MTAKATIFU
11 Oktoba 2026 na
MATANGAZO DOMINIKA YA 28 YA MWAKA A
St Peter's Catholic Church, Administrator
| Hakuna maoni bado


1. Usafi wa Kanisa

Tunawashukuru sana Jumuiya ya Mt. Maurus waliosafisha Kanisa jana. Idadi yao ni 15 Wiki ijayo ni zamu ya jumuiya ya Mt. Josephine Bakhita watafuatiwa na Jumuiya ya Mt. Monica.

2. Madarasa ya Kwanza ya Ekaristi na Kipaimara

Mafundisho ya Komuniyo ya kwanza na Kipaimara yataanza tarehe 17/10/2026, saa 2:00 asubuhi.

Kwa wale ambao hawajaandikisha wafanye hivyo na walioandikisha wahakikishe watoto wanahudhuria mafundisho.

3. Mwito wa Tenda kwa Huduma za Usalama wa Parokia

Parokia ya Mtakatifu Petro, Oysterbay inawaalika Wazabuni wenye sifa, uwezo pamoja na vigezo vingine muhimu kutoa huduma ya ulinzi katika eneo lote la Parokia kwa saa 24 kwa siku.

Nyaraka za Zabuni zenye maelekezo ya kina zinapatika Ofisi ya Parokia muda wa kazi kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi kuanzia tarehe 5/10/2026.

Gharama ya hati za tenda niTZS 50,000.

4. Hija kwa Wazee na Wastaafu

Hija ya Shirika la Wazee na Wastaafu -Jimbo iliyokuwa imeahirishwa tangu mwezi Juni 2026, sasa itafanyikia Pugu Jumamosi tarehe 17/09/2026.

Usajili unaendelea. Ada ya ushiriki niTZS 15,000, inayo cover kuingia kwenye eneo la Biblia kwenye Ardhi, vipaji, na chai.

Malipo yanapaswa kufanywa kupitia Benki ya Mkombozi kwa kutumia maelezo yafuatayo ya akaunti:

  • Nambari ya Akaunti: 00124319600501

  • Rejea ya Malipo:Hija Pugu Septemba 2026

Baada ya kufanya malipo, tafadhali tuma risiti yako ya malipo na jina lako kwa hazina wa chama cha ngazi ya parokia:

Adelina Msofe

Simu: 0652369867

Kila mtu anahimizwa kushiriki kwa wingi.

5. Sala ya Rozari kwenye Grotto

Sala ya Rozari kwenye Grotto inaendelea.

Kwa kuwa Misa Takatifu inaadhimishwa kila siku saa 5:30 AM, Rozari itaanza saa 4:45 AMili kuwapa washiriki fursa ya kuhudhuria Misa baadae.

Kuanzia tarehe 12/10 hadi 18/10 ni Kanda za Mtakatifu Mathayo Mwinjili na Mtakatifu Thomas Akwino.

6. Sasisho kuhusu Miradi ya Parokia

Michoro ya miradi ya Parokia imeshakamilika, na sasa kazi inayotekelezwa ni kufuatilia upatikanaji wa vibali vya ujenzi kwa mamlaka husika kwa ili kuwezesha utekelezaji wa miradi kuanza.

7. Radio Maria Tanzania – Kampeni ya Kikapu cha Mama 2026

Wana Utume wa Radio Maria Tanzania, wapo hapa Parokiani kwetu leo kwa ajili ya hamasa na kugawa bahasha za Kampeni ya Kapu la Mama 2026.

Wale ambao bado hawajapokea barua zao wanahimizwa kufanya hivyo. Tunatakiwa sote kuwakaribisha wageni kwa moyo mkunjufu na kuunga mkono kampeni.

Kauli mbiu ya Kampeni ya Kikapu cha Mama 2026ni:

“Upendo Ni Ushindi.”

8. Kutembelea Masista Wadogo huko Visiga

Katika 14 Oktoba, sikukuu ya kitaifa, wanachama waUWAKA, familia zao, na watu wote wenye mapenzi mema watatembelea Masista Wadogo huko Visiga.

Kila mtu anahimizwa kujiandikisha kupitia viongozi wa UWAKA katika ngazi ya jamii, eneo, au parokia.

Basi litakondoka kutoka parokia saa11:30 jioni.

Kila mtu anakaribishwa kwa moyo mkunjufu kujiunga na ziara, kuwasalimia Masista, na kujifunza zaidi kuhusu kazi na juhudi zao.

MATANGAZO YA NDOA

Kichapisho cha Kwanza

  • Kelvin Claudian Kajuna na Corolyne Hussein Kalinga

  • Gregory Peter Kilita na Consolatha Fabian Daudi

Kichapisho cha Pili

  • Nolasco Usulle Moshi na Judith Pedias Joctan

  • Joseph Nicodemus Sicilima na Laura Adelbert Mboki

  • Joseph Bhoke na Irene Charles

  • Erick Innocent Kakore na Esthre Elisante Mkumbo

  • Joseph Jonas na Mercy Lisa Katabazi

  • Mario Samwel na Happiness Karos

  • Augustine Alfred Masse na Ester Wilson Gwila

  • Deodath Erasmo na Neema Laurence Macha

  • Joachim Daniel Joachim na Jackline Joseph

  • Laurenti Fidelis na Adela Sostenes

  • Kevin Deogratius na Bona Julius

  • Kelvin Kizwald na Salome Budigila

  • Jonathan Pascal Norbert na Rose Clement Mkuwele

  • Simon Damas Luoga na Elizabeth Gasper Alexander Assey

Chapisho la Tatu

  • Andrea Mathias Vicent na Elizabeth Benedict Kihwili

ASANTE SANA KWA WEMA WAKO. MUNGU AKUBARIKI KWA WINGI.

MATANGAZO DOMINIKA YA 28 YA MWAKA A
St Peter's Catholic Church, Administrator 11 Oktoba 2026
Shiriki posti hii
Sign in to leave a comment