Matangazo ya Parokia
Tunawashukuru sana jumuiya ya Mt. Dominiko waliosafisha Kanisa jana. Idadi yao ni 27. Wiki ijayo ni zamu ya Jumuiya ya Mt. Martin wa Pores wakifuatiwa naJumuiya ya Mt. Polycarp.
Tunaendelea kuandikisha mafundisho kwa watu wazima(Wakatekumeni) ambao bado hawajapata fursa ya kupokea Sakramenti ya ubatizo, Ekaristi Takatifu na Kipaimara. Wenye uhitaji wafike ofisi ya Makatekista kuandikishwa siku za kazi huanzia saa 9:00 alasiri.
Tunaendelea kuandikisha mafundisho ya Komunio ya Kwanza na Kipaimara kwa lugha ya Kiingereza.
Kwa wanaotoka ndani ya Parokia waje na barua ya utambulisho kutoka jumuiyani pamoja na cheti cha ubatizo.
Kwa wanaotoka nje ya Parokia waje na barua ya utambulisho kutoka kwa Paroko wa Parokia wanakotokea pamoja na cheti cha ubatizo.
Dominika ya tarehe 18/01/2026 Mkurugenzi wa Vyama vya Kipapa Padri Alfred ataadhimisha Misa na kuhamasisha uchangiaji kwa vyama vya Kipapa. Dominika hiyo atagawa bahasha kwa lengo hilo. Tunaalikwa kumpokea kwa ukarimu.
Uchaguzi wa Utume wa Wazee na Wastaafu ngazi ya Parokia utafanyika Dominika ya tarehe 18/01/2026, mara baada ya Misa ya pili kwenye moja ya madarasa ya Parokia. Wajumbe wa Mkutano wa uchaguzi ni wajumbe watano kutoka kila Kanda. Tunaombwa kushiriki wote kwani ni chama pekee ambacho bado hazijakamilisha uchaguzi wa Viongozi.
Kwaya ya Moyo Mt wa Yesu ya hapa Parokiani, watazindua album ya nyimbo katika picha mjongeo(video) siku ya tar. 15/02/2026 kuanzia saa kumi kamili jioni.
Tiketi zinapatikana nje ya kanisa kwa:
TZS 30,000
TZS 50,000
TZS 100,000(VIP)
Meza ya VIP kwawatu 10 kwaTZS 1,000,000
Karibuni tuwaunge mkono katika uinjilishaji.