Skip to Content

ROHO NDIYO ITIAYO UZIMA

22 Januari 2026 na
ROHO NDIYO ITIAYO UZIMA
Sr. Violet Kwanungu LSOF
| Hakuna maoni bado

ROHO NDIYO ITIAYO UZIMA

“Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyokuambia ni roho, tena ni uzima.” (Yohane 6:63)

Hatuwezi kupata asali ikiwa hatuna mizinga ya nyuki, na wala hutuwezi kuvuna asali kama mizinga haina nyuki. Maisha bila sala, ni sawa na mwili bila roho, bila sala tunakufa kiroho ingawa tunapumua. Hatuwezi kuvikabili vita kama hatuna silaha za kupigana na wala hatuwezi kushinda vita, Mungu asipokuwa upande wetu. Bunduki bila risasi ndani yake haiwezi kumlinda mtu na maadui. Maisha bila sala ni sawa na kubeba bunduki isiyokuwa na risasi.

“Maana vita vyetu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwngu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu, wanaomiliki ulimwengu huu wa giza” (Waefeso 6:12)

Ni rahisi kukimbia ukiwa na nguvu, kuliko kukimbia ukiwa umechoka, sala itatupa nguvu ya kukimbia hata kama tumechoka. “Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika mweze kuyapinga mashambulizi ya adui; na mkiisha kupigana mpaka mwisho, mtakuwa bado imara.” (Waefeso 6:13

“Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka; bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.” (Isaya 40:29-31)

Gari haliwezi kwenda bila kuwa na matairi, maisha bila sala ni sawa na gari lisilo na matairi.Sala pekee ndiyo itakayotupa nguvu na ustahilivu wakati wa shida na majaribu mbalimbali ya maisha. Usichoke kuomba hata kama hujapata majibu ya shida yako, bado uko kwenye foleni wenda kesho Mungu atapokea maombi yako. “Si kwamba nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo, kwa ajili yake, nimeshikwa na Kristo Yesu.” (Wafilipi 3:12) 

katika Blog yetu
ROHO NDIYO ITIAYO UZIMA
Sr. Violet Kwanungu LSOF 22 Januari 2026
Shiriki posti hii
Madaraka
Sign in to leave a comment

Soma Inayofuata
OMBENI BILA KUKOMA