Skip to Content

YESU NIJALIE MOYO WA SALA

30 Januari 2026 na
YESU NIJALIE MOYO WA SALA
Sr. Violet Kwanungu LSOF
| Hakuna maoni bado

"Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohane alivyowafundisha wanafunzi wake." (Luka 11:1)

Ee Yesu, nijalie moyo wa sala nipate kusali kwa uchaji na imani thabiti.

Nijalie moyo wa sala nipate kusali kwa utulivu na usikivu.

Ee Yesu, nijalie moyo wa sala nipate kusali kwa moyo na kwa matumaini.

Nijalie moyo wa sala nipate kusali kwa unyenyekevu na upendo.

Ee Yesu, nijalie moyo wa sala nipate kusali wakati wa furaha na wakati wa shida na mahangaiko.

Nijalie moyo wa sala nipate kusali kila wakati na mahali popote.

Ee Yesu, nijalie moyo wa sala nipate kusali ningali hai na saa ya kufaa.

Amina.


katika Blog yetu
YESU NIJALIE MOYO WA SALA
Sr. Violet Kwanungu LSOF 30 Januari 2026
Shiriki posti hii
Madaraka
Sign in to leave a comment