Tunawashukuru sana Jumuiya ya Mt. Josephine Bakhita waliosafisha Kanisa jana. Idadi yao ni 15 Wiki ijayo ni zamu ya jumuiya ya Mt. Monica watafuatiwa naJumuiya ya Mt. Anthony wa Padua.
Parokia ya Mt. Petro, Oysterbay inawaalika Wazabuni wenye sifa, na vigezo vingine muhimu kutoa huduma ya ulinzi katika eneo lote la Parokia kwa saa 24 kwa siku. Nyaraka za Zabuni zenye maelekezo ya kina zinapatika Ofisi ya Parokia muda wa kazi kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi kuanzia tarehe 5/10/2026. Gharama ya nyaraka za zabuni ni shilingi 50,000/=, Mwisho kupokea maombi ni 30/10/2026.
SALA YA ROZARI KWENYE GROTO inaendelea. Kwa vile upo utaratibu wa Misa kila siku saa 11:30 Kwa msingi huo Sala ya Rozari itakuwa inaanza saa 10:45 (saa kumi na moja kasorobo).Ili kuwezesha washirikikuhudhuria Misa Kanda itakayoongoza Rozari kuanzia tarehe 19/10 hadi 25/10 ni Kanda ya Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili.
Uongozi wa Uwaka Parokia,unawashukuru sana wanaume wote pamoja na waamini wote na wote wenye mapenzi mema kwa kufanikisha michango ya kuwategemeza masista Dada wadogo. Parokia yetu imeshika nafasi ya kwanza katika Jimbo, Dekania na Parokia. Kipekee tunamshukuru sana Baba Paroko katika mafanikio hayo.
MATANGAZO YA NDOA
MATANGAZO YA PILI
Kelvin Claudian Kajuna na Corolyne Hussein Kalinga
Gregory Peter Kilita na Consolatha Fabian Daudi
MATANGAZO YA TATU
Nolasco Usulle Moshi na Judith Pedias Joctan
Joseph Nicodemus Sicilima na Laura Adelbert Mboki
Joseph Bhoke na Irene Charles
Erick Innocent Kakore na Esthre Elisante Mkumbo
Joseph Jonas na Mercy Lisa Katabazi
Mario Samwel na Happiness Karos
Augustine Alfred Masse na Ester Wilson Gwila
Deodath Erasmo na Neema Laurence Macha
Joachim Daniel Joachim na Jackline Joseph
Laurenti Fidelis na Adela Sostenes
Kevin Deogratius na Bona Julius
Kelvin Kizwald na Salome Budigila
Jonathan Pascal Norbert na Rose Clement Mkuwele
Simon Damas Luoga na Elizabeth Gasper Alexander Assey