Skip to Content

USIOGOPE MAANA NIMEKUKOMBOA

15 Desemba 2025 na
USIOGOPE MAANA NIMEKUKOMBOA
Sr. Violet Kwanungu LSOF
| Hakuna maoni bado

USIOGOPE, MAANA NIMEKUKOMBOWA


Usiogope kuendelea na safari ya maisha yako, hata kama njia yako ina giza na wala huoni mwanga mbele yako. Usigogope kuendelea na safari ya maisha yako, hata kama unapita mbugani kwenye wanyama wakali. Usiogope kuendelea na safari yako, hata kama unapita kwenye milima na mabonde. Usiogope kuendelea na safari yako, hata kama unahisi umeachwa peke yako. Usiogope kuendelea na safari yako, hata kama mvua ya mawe itakunyeshea zikiwemo na ngurumo za radi. Usiogope kuendelea na safari, hata kama njia ya maisha yako imejaa miiba. Usiogope kuendelea na safari, hata kama njia ya maisha yako ni jangwa. Usiogope kuendelea na safari yako, hata kama huijui kesho yako. Usiogope kuendelea na safari yako, hata kama unakabiliwa na vita vya kiroho.

"Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, ‘Usiogope maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu. Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; Na katika mito, haitakughalikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza. Maana mimi ni Bwana, Mungu wako; Mtakatifu wa Israel, mwokozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako. Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako.” (Isaya 43:1-4) “Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. Kwa maana mimi, Bwana, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia. Usiogope, Yakobo uliye mdudu, nanyi watu wa Israeli; mimi nitakusaidia, asema Bwana, na mkombozi wako ni Mtakatifu wa Israeli.” (Isaya 41:10, 13-14)

katika Blog yetu
USIOGOPE MAANA NIMEKUKOMBOA
Sr. Violet Kwanungu LSOF 15 Desemba 2025
Share this post
Tags
Sign in to leave a comment
BINADAMU SIO KITU PASIPO MUNGU KUMFANYA KUWA NI KITU